Ni Eneo Gani Ungependa Kupata Maarifa Zaidi?

Mahusiano.

Pata muongozo na ushauri kuhusu maisha ya mahusiano na ndoa na namna sahihi ya kuzikabili changamoto za mahusiano.

Afya Ya Akili

Pata msaada wa kisaikolojia kuhusu afya ya akili na mbinu mbali mbali za kuzikabili changamoto za afya ya akili.

Biashara

Tumia maarifa na mbinu mbalimbali za kisaikolojia katika kuvuta wateja kwenye biashara yako, kukuza mauzo na kuongeza kipato chako.

 

Ufahamu Ogonjwa Wa Kisaikolojia Wa NPD.

 

Ufahamu Ugonjwa Wa NPD (Narcissistic Personality Disorder) Ni Hatari Kwa Mahusiano Yako.

Kama Upo Kwenye Mahusiano Na Mtu Ambae Ana Shida Ya NPD Basi Sahau Kuhusu Furaha Kwenye Mahusiano Yako......

 

NPD Ni Tatizo La Kiakili Ambalo Linamfanya Mtu Kuwa Na Moyo Wa Kibinafsi, Na Kujiona Yeye Ni Bora Kuliko Wengine........

 

Yupo Tayari Kuathiri Mahusiano Yake Na Watu Wengine Yupo Tayari Kuwatoa Sadaka Watu Wengine Kwa Ajili Ya Manufaa Yake Binafsi........

 

Nafikiri Unamfahamu Vizuri MWIJAKU

 

Kwa Tabia Alizo Nazo Akili Yangu Inaniambia Huenda Akawa Na Hii Shida Ya Kiakili, Mfano Tukio La Kumuweka Sadaka Mke Wake Kwa Ajili Ya Mpila.

 

Mtu Mwenye Hii Shida Anajiona Yeye Ndio Mwenye Haki Zaidi Ya Kufanyiwa Mambo Mema Kwa Sababu Yeye Ni Bora.....

 

UTAMTAMBUA VIPI MTU HUYU

 

1. ONGEA YAKE : Mtu Mwenye Shida Hii Ya Kiakili Hupenda Kujiongelea Yeye Na Mara Nyingi Hupenda KujisifunKwa Uwezo Alio Nao Na Mambo Makubwa Alio Yafanya Au Anayoweza Kuyafanya..........

 

2. HAWEZI KUVUMILIA KUKOSOLEWA : Mtu Huyu Unapo Mkosoa Hupata Hasira Na Awaweza Hata Kukuchukia Kwasababu 

Hujiona Yeye Muda Wote Yupo Sahihi Na Hakosei......

 

3. UYONYAJI : Anapokuwa Kwenye Mahusiano Basi Mahusiano Yake Huyavuta Yawe Ya Upande Mmoja Yanayo Mnufaisha Yeye Pekee.

 

TABIA ZA MTU MWENYE UGONJWA WA NPD

1. KUJISIFU KUPITA KIASI : Atajisifu Akili Zake, Mafanikio Yake Au Urembo Wake Kupita Kiasi.

 

2. HAWANA HURUMA : Huwa Hawajali Kabisa Hisia Za Wengine Wanajali Zaidi Kuhusu Wao.....

 

3. WANAPENDA SIFA : Akili Yao Kubwa Wanaelekeza Kupata Attention Ya Watu, Hupenda Kusifiwa Na Hio Ndio Furaha Yao.

 

4. WABINAFSI

5. HUJIONA WAO NI BORA KULIKO WENGINE

 

CHAZO ZA TABIA

1. MALEZI : Kukuzwa Katika Mazingira Ambayo Mtoto Anapewa Kila Kitu Anachotaka Kwa Haraka Tena Bila Mipaka.....

 

2. KURITHI

3. MAZINGIRA YA KIJAMII: Shindikizo La Kijamii Au Matarajio Makubwa Anayopewa Na Jamii Inayo Mzunguka Huchangia.

JINSI YA KUKABILIANA NAO

 

1. MIPAKA: Ni Muhimu Kuweka Mipaka Ukiwa Kwenye Mahusiano Na Watu Wa Aina Hii....

 

2. KUJILINDA KIHISIA: Usuruhusi Tabia Zao Zikuvunje Moyo Au Kukunyima Amani Na Kukufanya Ujisikie Vibaya Kwa Kuwatambua.

 

3. MSAADA: Ukiona Tabia Zao Umeshindwa Kuzihimili Na Zinakupa Wakati Mgumu Tafuta Msaada Wa Kisaikolojia.

HITIMISHO

Kutambua Tatizo Ni Nusu Ya Kulimaliza, Hivyo Kuweza Kuishi Vizuri Na Watu Wenye Shida Ya NPD Hatua Ya Kwanza Ni Kuwatambua.